|
Jina: Rashid Matumla

Nafasi Yake: Bingwa wa dunia wa uzito wa kati (WBU)
Historia Fupi
Rashid Matumla alizaliwa mkoani Tanga hapo Mei 6, 1968. Aliingia katika masumbwi
mwaka 1979 ambapo ameshiriki mashindano mbali mbali kama vile ile ya olimpiki ya
Seoul 1988. Amewahi kuwa bondia bora Afrika mashariki na kati hapo mwaka 1990, na
mwaka huo huo alikuwa bingwa wa ridhaa Afrika mashariki na kati .
Mwaka 1997 alitwaa ubingwa wa Afrika na kutwaa taji la mabara linalotambuliwa
na WBU mwaka huo huo. Mwaka 1998 alitwaa taji la kimataifa WBU na mwaka hou huo
alitwaa ubingwa wa dunia wa WBU uzito wa lightmiddle.
Amecheza michezo 24 katika ndondi za kulipwa na ameshindwa mara moja. Kati ya
hiyo 14 ameshinda kwa knockout.
Makutano ya Rockers na familia ya Matumla January 1999
"Mafanikio ya akina Matumla ni jitahada za muda mrefu"
Kitu kilichochukuliwa kama burudani ya kawaida na Mzee Matumla miaka mingi iliyopita
leo hii kimegeuka kuwa sifa kwa taifa zima la Tanzania. Bondia huyo wa zamani, Mzee Matumla
anasema enzi hizo hakukuwa na chama ngumi hivyo mchjezo huo ulikuwa ni kwa ajili
ya burudani hasa kwa siku za jumapili huko katika mashamba ya mkonge Tanga.
Lakini mzee huyo alianza kubadili muelekeo wake katika ndondi pale pale alipoanza kuwafundisha
watoto wake mchezo huo. Si kwamba wanawe walikuwa wakiupenda mchezo huo ila nia
yake ilikuwa ni kuwaepusha na makundi ya kihuni. Hii iliwafanya wawe na nidhamau na
taratibu nao walianza kuvutiwa na mchezo huo. "Ilikuwa ikifika Jumapili kila mtu
anakasirika kwani siku hiyo itamaanisha kukimbia sana na mazoezi" anasema bingwa
wa dunia Rashid Matumla. Mzee Matumla aliendelea kuwakazania wanae katika masumbwi.
Lengo lake likiwa siku moja nao waje kuliletea taifa la Tanzania sifa, lengo ambalo
limetimia hivi karibuni. Mzee Mataumla anasema katika kupata mafanikio ni lazima
rasilimali itumike. "Lazima ugharamie mazoezi ili kupata timu nzuri, mimi niliwagharamia
sana hawa vijana kimazoezi, vifaa na kuwapa lishe ya kutosha. Kama huwapatii lisha
ya kutosha basi hujengi bali unaumiza". Mzee Matumla anaendelea kusema kuwa siri ya
mafanikio katika ngumi ni uvumilivu. "Kumbuka umapompata mwenzio, na yeye anakupata, mvumilivu
ndiye anashinda". Mzee Matumla anatoa wito kwa viongozi kuitumia vizuri sera ya michezo
vizuri, kuzingatia na kuweka mbele maslahi ya wanamichezo katika maandalizi ya awali
ili kutoa mabingwa kila wakati. "Kama hujala vizuri, utatetemeka tu".
Mzee Matumla anavutiwa na juhudi za bondia Marwa chni ya promota Madaraka Nyerere
na anasema kuwa vijana wengi wakipatiwa nafasi basi taifa litakuwa na mabondia wegi
katika nyanja za taifa na kulipwa.
Mzee Matumla anamshukuru sana promota Jamal Malinzi wa DJB Promotions kwa kuwapeleka
wanae katika anga za kimataifa. "Mimi niliwafikisha ngazi ya taifa, yeye kawapeleka
ngazi ya kimataifa". Hadi leo pamoja na kuwa Rashidi na Mbwana wanashikilia mikanda
ya dunia, Mzee Matumla bado hachoki kukagua mazoezi yao wawapo nyumbani.
"Nawakazania kuwa tayari wakati wowote kwani anaweza mtu kuja wakati wowote kutaka kuwa challenge,
hivyo lazima wawe tayari wakati wote", anamalizia mzee Matumla.
Rashidi Matumla anasema yeye bado hajaridhika kabisa na mafanikio aliyoyapata hivi
karibuni. Anasema lengo lake ni kushinda mataji yanayatambuliwa na vyama vingine
kama IBF, WBC au WBA. Anasema bidii yake katika WBU itamwenzesha kucheza WBC au WBO.
"Nikiweza kutetea taji hili mara mbili au tatu naweza kuomba kucheza kupitia vyama
vingine kama WBC au WBO" anasema Rashid. Anaendelea kusema kuwa katika ngumi kinachohitajika
ni nafasi, bila kupewa nafasi ya kupigana hautaendelea wala kutambulika.
Mafanikio ya akina Matumla yanatokana kwa kiwango kikubwa na kocha wao Norman
Hlabane wa Afrika ya Kusini. Rashid anasema wanapokuwa Afrika ya kusini huwa wanapata mazoezi mazito sana. Ansema anapokuwa nje ndio anakuwa makini zaidi hivyo hategemei kuweka kambi yake ya mazoezi
hapa Tanzania. Akiwa Afrika ya Kusikni huwa anakuwa na program nzuri ya mazoezi.
Hii yote inatokana na kuwa na kocha mzuri na mwenye kuipenda kazi yake. "Kocha wangu
ni mtu mkali sana kuhusu mazoezi" anaongeza Rashid. Kocha huyo huwajenga ki boxing
na kisaikolojia. "Tukiwa nyumbani tunakuwa kama watoto wake lakini mazoezini anabadilika
kabisa". Rashid anamsifia kocha wake kwa kusema kuwa ni mtu makini na ndio maana
ametoa mabingwa wa dunia kama watatu auwnne hivi. "Kila siku atakuotoa
makosa, ukifanya vizuri anakwambia na vibaya anakwambia". Kutokana na mazoezi ya kocha wake
huyo hivi sasa anajisikia nguvu zaidi tofauti na mwanzo ambapo alikuwa mwepesi
lakini hana nguvu. "Ukipata mafunzo Afrika ya kusini una uwezo wa kupigana na mtu
yeyote duniani", anasema Rashid.
Anavutiwa na mchezo wa Moses Marwa na ndiye bondia ambaye anamuona anaweza kufanya
vizuri katika ndondi za kulipwa, pamoja na umri wake. "Mbona Foreman alirudi kama mtu
mzima na alifanya mavitu ?" anauliza Matumla.
Kimataifa alikuwa anavutiwa na Mohammed Alli na Sugar Ray Leonard. Hivi sasa anavutiwa
na Roy Jones.
Nukuu muhimu
"Huwa sina makeke. Mimi ni wa vitendo sio mtu wa porojo".
"Ubingwa wa dunia haunifanyi nijione tofauti na watu wengine. Ninafurahia heshima
ninayoipata kutoka kwa watanzania wenzangu. Hata hivyo mimi bado ni mtu yule
yule, naishi kule kuloe nilikokuwa nikiishi, naongea na watu wale wale na natembelea
sehemu zile zile".
"Mbwana ni bondia mzuri anaachohitaji ni nafasi tu. Kule Afrika ya Kusini watu
walikua wakihama hata Gym kumkimbia. Ni mwepesi sana."
"Mzee wetu alifanya boxing kama elimu. Akiwa off kazini, tulikuwa tunaenda nae
mazoezini, wakati mwingine tulikuwa tunamkimbia. Tulikuwa tukiwasikia akina Nassor
Michael na Isangura tulitamani kuwa kama wao na baba yetu alikuwa akitupa moyo sana."
"Jioni tulikuwa tunatembea toka klabu ya Simba mpaka nyumbani (keko) kwa miguu
na njia nzima anakuwa akitutoa makosa. Ulikuwa unafanya bidii ili nyumbani
usikosolewe".
^^^^^^^^ ^^^^^^^^
NEXT
|
 |